Saturday, May 20, 2017

Nyota 10 wa kike wanaopendwa Nollywood hawa hapa


TAASISI ya Ushauri ya NOI Global, imefanya uchunguzi na kutaja wasanii nyota 10 wa kike nchini hapa wanaopendwa zaidi katika tasnia hiyo.
Uchunguzi huo ulifanywa kwa kuwakusanya wadau mbalimbali wa filamu na kuwapigia kura wasanii wanaowaona wanapendwa.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi huo, wadau wengi walisema wanafurahia kuangalia zaidi filamu za Nollywood kuliko vitu vingine.
Asilimia 39 wanapenda kuangalia filamu za mapenzi za kuchekesha, asilimia 40 vichekesho na asilimia 14 wanapenda filamu za mapenzi tu.
Ilielezwa filamu itapendwa zaidi endapo mshiriki atakuwa msanii wa kike au kuume ambaye ni maarufu katika jamii.
Pamoja na hali hiyo lakini wengi wa walioulizwa walisema asilimia 48 ya Wanaigeria wanapenda kuangalia filamu za Nollywood ila wanapaswa kuboresha utunzi wao.
Wasanii hao 10 waliotajwa katika uchunguzi huo ni Genevieve Nnaji, Mercy Johnson, Omotola Jalade, Funke Akindele, Ini Edo, Patience Ozokwor, Mercy Aigbe, Stephanie Okereke, Chika Ike na Fathia Balogun.

0 Comments: