Friday, May 5, 2017

Vanessa Mdee ‘amkoromea’ anayemchafua kila kukicha

MSANII Vanessa Mdee amesema kuna msanii mkongwe anayemheshimu kwenye mzuiki wa kizazi kipya lakini amekuwa na tabia ya kumchafua mara kwa mara.
Mdee ambaye amekuwa maarufu kutoka na nyimbo zake mbalimbali ameamua kutumia mtandao wake wa kijamii kutoa la moyoni baada ya kuona ni bora aseme kuhusu huyo msanii anayefanya kazi ya kumchafua.
 “Inasikitisha mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa lakini kila kukicha jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka.Siwezi kujibishana na wewe itakuwa utovu wa nidhamu baba,” ameandika Vanessa Mdee.

0 Comments: