Friday, May 5, 2017

Nay tayari aufanyia kazi ushauri wa JPM tekeleza ombi la JPM


RAPA Nay wa Mitego amesema ameufanyia kazi ushauri wa Rais John Magufuli kuhusu wimbo wake wa Wapo ambapo ameweka wazi remix ya wimbo huo ipo mbioni kutoka.
Awali wimbo huo ulifungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), lakini baadae Rais Magufuli aliruhusu wimbo huo uelendelee kupigwa kwani anaupenda lakini akashauri msanii huyo aongezee baadhi ya mambo muhimu.
“Wimbo wa Rais umekamilika na muda wowote unaweza kutoka. Nimeongeza mambo mengi ndani yake, kwa hiyo mashabiki wa muziki wasubiri na muda si mrefu watausikia,”anasema.
Nay wa Mitego pia ametumia nafasi hiyo kuwataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumuunga mkono katika muziki wake.


0 Comments: