Saturday, May 20, 2017

Shamsa Ford awapa somo mastaa wa kike


MWIGIZAJI wa filamu nchini Shamsa Ford amewabwatukia mastaa wa wanawake waache tabia za kuchagua wanaume wa kuwaoa, kwani leo wana majina makubwa na wanaonekana warembo lakini ipo siku itafika hata hao wanaume wanaowatongoza leo watapotea kabisa.
Akizungumza wiki hii, Shamsa Ford anasema kwa sasa wanawake wenye majina makubwa wanajiona warembo kiasi hufikia hatua hata ya kusubiri wanaume matajiri wa kuwaoa bila kukumbuka kuwa hata hao matajiri wana watu wao.
“Wasichana wenzangu maisha ni mafupi , leo tunavuma na kupendwa kila kona tunapokatiza ila kuna muda utafika hata nzi hakusogelei.Hata uwe mzuri na maarufu kiasi gani lakini ndoa ina heshima yake.
“Msiwe wachaguzi sana, maana ukisema unamsubili tajiri aje akuoe na yeye huyo tajiri ana mwanamke wake aliyetoka naye mbali kimaisha,”anasema Shamsa kwenye ukurasa wake wa Instagram,”anasema.
Anafafanua ni muhimu kumuomba Mungu akupe mwanaume mwenye kumjua Mungu, mwenye upendo, heshima, mtafutaji hayo mengine yanakuja tu. Nguvu ya mmoja ni tofauti na ya wawili,”anasema.Shamsa Ford kwa sasa yupo kwenye ndoa na mfanyabiashara Chidi Mapenzi.

0 Comments: