Saturday, May 20, 2017

Amber Rose anusurika na msala wa Kibaka



KICHUDA mwenye kismati cha kutoka na Masupastaa nchini Marekani, Amber Rose amesema anahisi kuna mtu alimvamia nyumbani kwake na kulala Zaidi ya masaa manne.
Inasemekana nyumba ya Amber iliyopo maeneo ya San Fernando Valley ilivamiwa na kibaka huyo siku ya Jumatano ambapo alipitia dirishani maeneo ya jikoni kabla ya kuzama katika vyumba vya nyumba hiyo.
Amber ambaye anaishi na mwanae aliyezaa na Rapa, Wiz Khalifa na Mama yake aliwapigia simu Polisi ambao walifika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa tukio hilo licha ya kubaini kutoibiwa kitu chochote.

0 Comments: