Saturday, May 20, 2017

‘Sipendi wanaume wafupi’ -Shilole



MSANII wa Bongo Fleva, Shilole ameamua kutaja sifa za mwanaume anayempenda na kusema kuwa anavutiwa sana na wanaume warefu kuliko wafupi.
Shilole anasema mesema anampenda mwanaume yoyote yule anaejitambua ingawaje kidogo sifa za nje awe mrefu kwani hana hisia zozote kwa mwanaume mfupi.
“Napenda mwanaume yoyote yule ilimradi anajitambua basi, suala la muonekano hilo linatengenezwa ila kiukweli kabisa napenda sana mwanaume mrefu, mwanaume mfupi kwangu hapana.
“Sipendi wanaume wafupi, Barnaba yeye ni mfupi na kila mmoja ameumbwa na Mungu tofauti. Ila sasa hivi vigezo na masharti kuzingatiwa,”anasema Shilole.
Anaongeza kwa sasa anatamani sana kuolewa kwani ndoa ni heshima kwa mwanamke .
“Hamna mtu asiyependa kuolewa, ndoa ni heshima ndiyo maana unasikia watu wanasema mke wa fulani yule, muwe wa fulani yule lakini siyo aah yule si mwanamke tu kwa hiyo ndoa ni heshima” anasema Shilole.

0 Comments: