Friday, May 19, 2017

Sapraizi yailipua furaha ya Damilola


KIMWANA Damilola Adegbite amekuwa mtu mwenye furaha mwishoni mwa wiki hii baada ya mumewe, Chris Attoh kumfanyia Sapraizi katika siku yake ya kuzaliwa huku akimuandikia maneno ya kimapenzi kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Attoh aliandaa sherehe fupi ya kumpongeza Damilola kwa kufikisha umri mwingine bila kumueleza na kuwashirikisha marafiki zao wa karibu huku sapraizi hiyo ikimaliza tetesi za kwamba wawili hao walikuwa kwenye mpango wa kumwagana baada ya kudumu kwa miaka miwili.
“ Asante Baba, Asante Mume wangu kwa zawadi hii kubwa uliyonipa siku ya leo, umenifanya nijisikie wa kipekee duniani, naamini sasa wale ambao walikuwa wakieneza stori zao uongo watakuwa wametumbua mimacho kwa aibu,” aliandika Damilola katika ukurasa wake.


0 Comments: