SIJALI wanachosema! Ndiyo kauli ambayo mrembo Bonang Matheba ameitoa wiki hii akisema hajali kinachozungumzwa mitandaoni kuhusu yeye zaidi anawaza kukamua zaidi kazi ili azidi kufanikiwa.
Bonang anasema anachoamini yeye hakuna binadamu ambaye anakosa wapinzani na maadui hivyo hajali chochote pale anapoona maneno mabaya yanayozungumzwa dhidi yake.
“ Nafikiri sasa nimekuwa na wala sipati shida na maneno ya mitandaoni, mwanzoni nilikuwa mtu naeumizwa na maneno ya watu na hata kufikia hatua ya kujifungia chumbani na kulia machozi, lakini baadae nikagundua nikiwapa nafasi ya kuniumiza watajiona washindi, hivi sasa nawapuuza tu,” anasema Bonang.
0 Comments:
Post a Comment