Friday, May 5, 2017

Rick Ross amaliza bifu la Drake, Meek

KIRANJA wa Lebo ya Mayback Music, Rapa Rick Ross amewatonya Drake na hasimu wake Meek Mill kuwa siyo ishu kuwa na bifu badala yake wapige kazi na kuachia ngoma ambazo zitawakonga mashabiki wao.
Ross aliyasema hayo wakati alipokutana na wakali hao wawili ambapo licha ya kufanya mazungumzo nao ambapo aliwapatanisha na kuamua kuweka tofauti zao pembeni na sasa wanasonga mbele.
Bifu la wawili hao lilichagizwa zaidi na uhusiano wa Meek na Nikki Minaj na hiyo ni kutokana na Drake kutajwa kuwahi kutoka kimapenzi na mrembo huyo.
“ Hakuna bifu tena tumezungumza wote pamoja na kukubaliana kumaliza tofauti zilizokuwepo, huu siyo muda wa bifu, huu ni muda wa kupiga pesa,”anasema Ross.


0 Comments: