Friday, May 5, 2017

Jaden Smith aamua kukomalia muziki


KUTOKA familia ya kishua, Jaden Smith ambaye ni Mtoto wa Supastaa Will Smith amesanua kuwa yupo mbioni kuachia ngoma yake ndani ya wiki mbili zijazo.
Jaden ambaye pia ni muigizaji akitamba na movie ya Karate Kid, amesema kwa sasa amepanga kuingia katika muziki kwa nguvu kubwa ambapo ngoma yake hii ya Batman anaona itafungua mianya ya kukua kimuziki zaidi.
“ Sio kwamba nimeacha kucheza filamu, hapa tunavyozungumza nakamilisha filamu yangu ya Life in a Year niliyocheza na Cara, kwa sasa nataka kuachia ngoma hii ambapo baadae ntaachia albamu yangu kamili iitwayo, Syre,” anasema Jaden.


0 Comments: