Saturday, May 13, 2017

Renny amzuia babaye kumtakia heri ya kuzaliwa


MSANII mkongwe wa filamu nchini Nigeria, Segum Arinze, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumtakia heri ya kuzaliwa mwanaye, Renny lakini mtoto huyo alimzodoa kwa kuambiwa asirudie tena kufanya hivyo.
Arinze, 51 alifanya hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliweka picha ya mtoto huyo, 20 na kumuandikia maneno ya kumtia moyo ili afanikiwe katika maisha yake.
Lakini chakusikitisha Renny alimjibu baba yake kwa kumwambia:” Kitu kimoja unapaswa kujua, kwanza mama yangu haitwi Ann ila ni Anne. Sihitaji ujifanywe mwema kwangu na uache kuzungumza uongo”. Baada ya hapo alifuta huo ujumbe.
Kitu hicho kiliibua mjadala mkubwa katika ukurasa wa Arinze kitu ambacho hadi sasa haijaeleweka nini kinaendelea.


0 Comments: