Saturday, May 13, 2017

Huddah Munrose amtolea uvivu msanii Nigeria


MSHIRIKI wa zamani wa Big Brother, Huddah Munrose, amemtolea uvivu msanii wa filamu wa Nigeria, Mercy Aigbe ambaye alimtukana akimuhusisha kutoka kimapenzi na muwe wake, Lanre Gentury kwa kumwambia anapaswa alaumiwe kama mambo yatakwenda kombo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Huddah aliandika:”Unaendelea kutukana na kulalamika unapigwa wakati bado upo katika ndoa kwa miaka 10”.
Aliendelea:”Nimekulia katika maisha ya kutukanwa nikiwa nyumbani na niliambiwa siku mwanaume akikupiga, atakupiga tena. Hivyo hupaswi kuendelea kubaki ni bora uondoke haraka.
Alisema kuendelea kuweka wazi mambo yako katika mtandao wa kijamii haikusaidii na kwamba wakati mwingine jifunze kutatua matatizo yako mwenyewe.


0 Comments: