Saturday, May 13, 2017

Omotola ataka ‘ambulance’ iachwe ipite


MSANII nguli wa filamu nchini Nigeria, Omotola Jalade, amewaomba madereva nchini humo kupisha njia wakati gari ya wagonjwa (ambulance) inapokuwa inapeleka wagonjwa hospitalini kutibiwa.
Omotola ambaye ni mama wa watoto wanne, aliweka katika ukurasa wake wa Instagram na kuwataka madereva hao kutoa ushirikiano kwani wakati mwingine hubeba wagonjwa mahututi.
Kupitia ukurasa wake huo aliandika:” Madereva na mashabiki wangu, endpo utaona gari ya wagonjwa jaribu kuipisha, tafadhali! tafadhali! hakikisha unaacha njia ili ipite kwa urahisi”.
“Mara nyingi gari hiyo hubeba wagonjwa mahututi, hivyo kama utakuwa katika baiskeli, pikipiki au gari hakikisha unaisaidia kwa kuacha njia wazi lakini ukiendelea kukaidi na kuichelewesha utasababisha mgonjwa kupoteza maisha”.


0 Comments: