Friday, May 12, 2017

Priyanka awataja wawili anaowakubali

SUPASTAA kutoka kiwanda cha filamu nchini India, Priyanka Chopra ameamua kuonesha mapenzi yake kwa Wanaharakati mashuhuri duniani, Mahatma Gandhi (India) na Nelson Mandela (Afrika Kusini).
Priyanka amesema wanaharakati hao wamefanya makubwa katika Nchi zao kiasi cha kubaki kama alama ya ukumbusho wa mataifa yao kwa jinsi walivyopigania Uhuru na Demokrasia.
“ Wawili hawa walipigania haki ya raia wote duniani bila kujali itikadi zao za kidini wala rangi zao, walijali utu na walikuwa tayari kupoteza maisha yao kwa ajili yaw engine, sisemi hivi kwa sababu nimezaliwa tarehe moja na Mandela lakini namzungumzia kama mtu aliyeacha urithi mkubwa kwa Taifa lake,” alisema.


0 Comments: