Friday, May 12, 2017

Mambo yazidi kumnyookea Salma Mumin


SANAA inalipa bwana wee! Unaambiwa mrembo Salma Mumin amekula shavu refu baada ya kusaini mkataba na taasisi Ph8 inayojishughulisha na masuala ya Afya, Maji safi na Chakula.
Taasisi hiyo iliyopo jijini Los Angeles, Marekani imeingia makubaliano na Kimwana huyo ya kuwa balozi wao baada ya kujiridhisha kuwa anazo sifa za kuwa balozi wao nchini Ghana.
“Salma amekidhi vigezo vyote vya kuwa Balozi wetu, ni binti mrembo ambaye anajiamini na kupitia yeye taasisi yetu inaamini itaweza kusonga mbele kupitia yeye,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


0 Comments: