Friday, May 12, 2017

Diesel na The Rocky sasa mambo shega


HALI shwari Mwanangu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya wakali wawili wanaotamba na filamu yao mpya ya Fast Furious, Vin Diesel na The Rocky kuamua kumaliza bifu lao la muda mrefu.
Wawili hao ambao wameshirikiana katika filamu za Fast Furious kuanzia sehemu ya kwanza hadi hii mpya ya nane walikuwa na bifu zito kiasi kwamba ilifikia hatua Vin Diesel kutamka kwamba hata kwenye maisha ya kawaida The Rocky hawezi kumpiga.
Lakini katika hali iliyoashiria bifu hilo sasa limekwisha katikati ya wiki hii, Vin Diesel alituma ujumbe wa kumtakia maisha marefu The Rocky katika siku yake ya kuzaliwa na kuandika
“ Nikitazama ni mangapi tumeyafanya ni mangapi tumeshikana bega kwa bega ili kufanikisha hata yale yasiyowezekana, Najivunia sana kuwa na wewe,” Alisema.


0 Comments: