Saturday, May 13, 2017

Davido apata mtoto wa pili

 
MSANII wa muziki nchini Nigeria, Davido, amepata mtoto wa pili na mpenzi wake raia wa Marekani, Amanda.
Davido aliteka hisia za mashabiki wake kupitia mtandano wake wa Kijamii wa SnapChat, katikati ya wiki kwa kutoa taarifa hiyo huku akisema mwanaye huyo wa kike anaitw Hailey.
Msanii huyo alikwenda kumuangalia mpenzi wake hospitalini kabla ya kujifungua aliwaomba mashabiki wake waseme neno lolote la kumuombea ajifungue salama kupitia ukurasa wake huyo.
Mama wa mtoto huyo maisha yake yapo Atlanta nchini Marekani.


0 Comments: