Tuesday, May 16, 2017

Msaga Sumu akamilisha Mwanaume mashine

MKALI wa muziki wa Singeli nchini, Msaga Sumu ameachia wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la Mwanaume Mashine huku akieleza kibao hicho ni kwa ajili ya wanaume wote wanaojituma kwenye kazi.
Akizungumza wiki hii, msanii huyo amewaaambia mashabiki wake wategemee video ya wimbo huo ndani ya siku saba kuanzia sasa na amejipanga kivinge ili kuwaletea burudani ya kukata na shoka ingawa upande wa management bado mambo hayajawa katika kiwango kile kinachotakiwa.
Amefafanua kuwa kupitia muziki wa singeli umemjengea heshima kubwa ingawa mwanzoni kuna watu walikuwa hawamuelewi lakini sasa kitu ambacho anaweza kujivunia.
“Muziki huu umenifanya nimeenda kumpa tuzo Isha Mashauzi mbele ya wageni na viongozi kibao, muziki huu pia umenitembeza nchi nzima,” anasema.
Anaongeza kwa sasa ana uhakika muziki wake umeshika kasi mikoani na si Dar es Salaam peke yake.

0 Comments: