Tuesday, May 16, 2017

Wingi wa mashabiki wa Chura wamfurahisha Snura

MSANII wa muziki Bongo Snura Mushi a.k.a Snura amefurahishwa na mashabiki aliowapata wakati anatoa nyimbo ya chura mwaka jana mwezi wa nne.
Snura ameeleza kufurahishwa kwa kuongeza idadi ya mashabiki hao kuwa wimbo yake ya chura ilimuwezesha kupata mashabiki wengi katika soko lake la muziki na anaimani bado anao mashabiki zake hao ambao wanaongezeka.
“Nilishitushwa sana na producer Don Jazzy alivyo post video anaimba nyimbo yangu ya chura, nakumbuka aliposti pia hata video yake kwenye Instagram yake,
“Pia meneja wake Lil Wayne alipost pia nyimbo ya chura nilifurahi kuona watu wameielewa,”anasema Snura.
Nyimbo ya chura ilifungiwa na BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) mwezi wa tano, kutokana na kukosa maadili.

0 Comments: