Tuesday, May 16, 2017

Ali Kiba kuingiza bidhaa zake sokoni

MFALME wa Bongo Fleva , Ali Kiba a.k.a King Kiba ametangaza ujio wa bidhaa mbalimbali kutoka katika brand yake ‘AK’  na ‘King Kiba’.
Akizungumza wiki hii, Kiba anasema kuwa hiyo ni mipango mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alitoa baadhi ya bidhaa kama promotion.
“AK ni brand ya Ali Kiba, nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote,”anasema Kiba.
Anaongeza “Kuna malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna jeans, viatu na glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink”.
Siku za karibuni mwimbaji wa muziki huo Diamond Platnumz naye  alizindua manukato yake yake yanayofahamika Chibu Perfume.

0 Comments: