Friday, May 12, 2017

Kesi ya Thato yasogezwa mbele


EBWANA jumba bovu limemuangukia mkali wa filamu kunako ardhi ya Madiba, Thato Molamu baada ya kufikishwa mahakamani jijini Pretoria baada ya kukamatwa akiendesha gari akiwa amelewa.
Thato akiwa anaendesha gari yake aina ya Jaguar alikamatwa Jumatatu ya wiki hii katika kona ya Nelson Mandela, Sunnyside Pretoria na alipelekwa kituo cha Polisi ambacho aliwekwa ndani kabla ya kutoka baada ya kulipa kiasi cha Randi 1,000.
“Kesi imeahirishwa hadi Juni 19 ili kupisha uchunguzi zaidi , mahakama imeruhusu Polisi kuendelea kufanya uchunguzi ili ikifika mahakamani iwe na ushahidi uliokamilika,” alisema Msemaji wa Polisi, Daniel Mavimbele.


0 Comments: