Friday, May 5, 2017

Amanda na Afrique kumbe hawajaachana

AMANDA Acquah amebainisha kuwa licha ya yeye na mume wake, Afrique Acquah kutengana bado ni wanandoa kisheria hivyo hana haraka ya kuingia kwenye mahusiano mapya.
Staa huyo wa filamu aliolewa na Mwanasoka wa Timu ya Taifa ya Ghana, Afrique lakini amesema kukosa kwao uzoefu wa mahusiano ndio kulichangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kuelewana hali iliyopelekea kutengana.
“ Bado sisi ni wanandoa na hilo halina ubishi, skendo ambazo zimekuwa zikivumishwa kuhusu sisi bado haimaanishi kuwa inavunja ndoa yetu, tulihitaji kupeana nafasi ili kila mmoja wetu ajitathimini na tukirudiana kila mmoja wetu awe ametulia na kulea familia yetu,” anasema Amanda.

0 Comments: