Saturday, May 6, 2017

Iyke akiri mapenzi yake kwa Rita


SUPASTAA Jim Iyke ameweka hadharani kuwa hujisikia fahari na furaha zaidi anapocheza filamu za kimapenzi akiwa kama mwanaume wake kisura Rita Dominic.
Iyke ambaye anatamba na filamu yake ya My first Wife aliocheza na Rita alisema amekuwa akifurahia kucheza na mrembo huyo kutokana na umahiri wake wa kuvaa uhusika na ubunifu alionao.
“Hakuna chochote kati yetu zaidi ya ushikaji wa kazi ambao tumekuwa nao, Rita ni mtu ambaye napenda kufanya nae kazi, ananifurahisha kwa ubora wake na ubunifu alionao zaidi anajua jinsi ya kucheza na mimi,” anasema Iyke.

0 Comments: