Saturday, May 6, 2017

‘Hakuna mwanaume anaweza kunitongoza’

NI kama amewatolea maneno ya dharau wanaume, unaambiwa Kimwana Yvonne Okoro ametoa kauli ngumu baada ya kusema hakuna mwanaume anaweza kumtongoza.
Kujiamini huko kwa Yvonne kunatokana na uwezo wake wa kubuni vitu mawazo mbalimbali ambayo yamekuwa yakimsaidia kuanzisha biashara zake huku akiwa na uwezo wa kuandaa filamu zake mwenyewe jambo ambalo anaamini linamuweka daraja la juu zaidi.
“Unajua siyo kwamba wanaogopa kunitafuta kwa sababu eti natisha au nawajibu vibaya lakini wanaamini mimi ni mwanamke wa daraja la juu.
“Watu wamekuwa na mawazo ya ajabu sana juu yangu wakifikiri kwa vile ninajiweza kiuchumi basi sitakiwi kuwa na mwanaume, jamani naombeni msiniogope,” anasema Yvonne.

0 Comments: