Saturday, May 6, 2017

Rita: Jamani sina muda wa kuolewa


KIFACE kunako kiwanda cha filamu za Nollywood, Rita Dominic amezidi kuwakata mdomo wanaume wote wakware baada ya kusema kwa sasa hahitaji kuingia kwenye mahusiano na anafurahia maisha ya kuwa singo.
Rita mwenye umri wa miaka 41 amesanua kama angekuwa anahitaji kuolewa basi angeolewa miaka mingi iliyopita kutokana na msururu wa wanaume ambao wamekuwa wakimfuatilia lakini binafsi anafurahia kuishi mwenyewe bila kuwa na Mwanaume.
“Daima nimekuwa nikifanya maamuzi ya maisha yangu bila kujali watu wanaonizunguka wanataka nini, mimi kuoelewa inawezekana lakini ni pale ambapo nafsi yangu itaridhia siyo kwa sababu mashabiki wangu wanataka,” anasema Rita.


0 Comments: