Saturday, May 6, 2017

Ini Dima azidi kutamba na uzuri wake

EBWANA King’asti Ini Dima-Okojie amezidi kuacha gumzo katika mitandao ya kijamii kutokana na kauli zake tata ambazo amekuwa akizitoa ambapo safari yeye ametoa kali nyingine baada ya kusema hakuna mrembo kama yeye Nollywood.
Ini Dima amesanua kuwa kujiweka tofauti na kuwa mbunifu katika urembo ndio kumekuwa kukimfanya aamini hayupo mrembo kama yeye katika kundi kubwa la mastaa wa filamu nchini Nigeria.
“Wapo wasichana wazuri ndani ya Nollywood lakini hakuna ambaye yupo juu yangu, najijua mimi ni mrembo kiasi gani, na nimekuwa nikizidi kuwa mzuri kadri siku zinavyozidi kusonga,” alijitapa Ini.

0 Comments: