Saturday, May 6, 2017

Kumbe hawana bifu lolote, wanatuzuga


STAA wa filamu Eniola Badmus amesema hakuna bifu lolote kati yake na mkali mwenzake Funke Akindele huku akikasirishwa na namna ambavyo vyombo vya habari vinakuza uvumi huo.
“Sijui hizi taarifa za bifu kati yangu na Funke zimetoka wapi, hatujawahi kugombana wala kupishana kauli na ni mtu ambaye tunaheshimiana sana, na taarifa zote ambazo zinatolewa kuhusu sisi ni uzushi,” anasema Eniola.
Stori za wawili hao zilianza kuenea baada ya Funke kutokufika katika msiba wa Baba yake Eniola. Lakini wawili hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikanusha kutokuwa na ugomvi.


0 Comments: