Friday, May 5, 2017

Harmorapa achimba mkwara mzito


MSANII Harmorapa amechimba mkwara mzito kwa wasanii wenzake kuwa wimbo wake unaofuta kwa sasa utakuja kupoteza nyimbo zao.
Harmorapa amesema ngoma yake mpya itafunika wasanii wote wakubwa barani Afrika na kusisitiza ni vyema wakaachia ngoma zao kwa muda huu, kwani wakichelewa huenda wakapatwa na bomu hilo ambalo litawafanya wasisikike kabisa kwenye ramani ya muziki.
“Mashabiki wangu nawaletea bomu litakalo sambaratisha ngoma za wasanii wote Afrika, kwa hiyo nawakanya na wasanii wote Afrika walioficha vinyimbo vyao ndani wavitoe haraka hivi sasa kabla ya kabla mimi sijaachia bomu langu kwani nikiachia hamto sikika tena,”anasema.


0 Comments: