Friday, May 5, 2017

Bipasha amwagia sifa lukuki mumewe

MAHABA niue niponde ponde kama nyanya! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mrembo Bipasha Basu kummwagia sifa za kutosha mume wake ambaye pia ni staa, Karan Singh kuwa hakukosea kuolewa nae.
Wawili hao ambao wamekuwa wakicheza filamu pamoja wamekuwa wakitajwa kama wanandoa wanaokuja kwa kasi katika ulingo wa filamu kutokana na ubora wa kazi ambazo wameshiriki hadi sasa.
“ Maisha yamebadilika sana tangu tumeoana, na namshukuru Mungu kwa kunipatia mume ambaye ni rafiki, mfanyakazi mwenzangu na mwalimu bora, mwaka mmoja wa ndoa yetu umejawa mafanikio ambayo tunaamini yatazidi siku hadi siku,” anasema Bipasha.


0 Comments: