Friday, May 12, 2017

Kumbe malengo ya Amit yametimia!


AMIT Sadh amefichua kuwa halikuwa jambo la kawaida pale alipofanikisha filamu yake aliyocheza na Nguli wa filamu nchini humo, Amitabh Bachchan kwani ni nafasi aliyoitamani kwa muda mrefu.
Akizungumzia filamu hiyo ambayo ameiachia wiki hii na kucheza kama Mjukuu wa Veterani huyo, Amit ameeleza kwamba baada ya kuteseka kwa muda mrefu katika maisha yake ya uigizaji sasa anaamini njia ya mafanikio inaanza kufunguka.
“Ni jambo kubwa katika maisha yangu ya sanaa, najivunia kuwa mmoja wa waigizaji waliofanya kazi na Bachchan, ni mtu poa ambaye kwetu amebaki kuwa alama ya Bollywood, sasa naamini waliokuwa hawaniamini watakosa la kuongea,” anasema Amit.


0 Comments: