MSANII nguli wa Nollywood, Chifu Ngozi Ezeonu amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 52 huku akiwa amecheza filamu 150.
Msanii huyo alisherehekea siku hiyo juzi akizaliwa mwaka 1965 katika mji wa Anambra nchini Nigeria.
Mwanamama huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mwandishi wa Habari, alianza kufanya kazi hizo za kisanii mwaka 2002 akiongoza Adesuwa na tangu hapo amekuwa akifanya vizuri katika kazi zake.
Tangu kipindi hicho hadi sasa, nyota huyo amefanikiwa kucheza filamu 150 na bado anaendelea kutengeneza zingine.
0 Comments:
Post a Comment