MSANII nyota wa Nollywood, Tonto Dikeh amejikuta katika wakati mgumu baada ya mashabiki wake kumpa somo kuntu kuhusu masuala ya ndoa.
Staa huyo aliachana na mumewe mwezi uliopita kutokana na madai kwamba alikuwa akipigwa na masuala mengine mbalimbali.
Kwa mujibu wa ushauri aliopewa kupitia ukurasa wake wa Instagram, nyota huyo alitakiwa kuwa mvumilivu katika ndoa na si kuendekeza ujana.
“Unaweza kumuweka chura katika sufuria alafu weka maji, utakapochemsha hayo maji na chura yupo ndani atabadili joto lake ili aishi kadri maji yatakavyozidi kupata joto, lakini mwisho wa siku akiona yanazidi hana budi kutafuta njia ya kutoka nje,” ilieleza sehemu ya ujumbe aliopewa na kuendelea;
“Akifanikiwa chura kutoka nje atakuwa ameshapoteza uwezo wake wa kurudi katika hali yake ya kawaida hivyo atafariki dunia, mwisho wa siku tutajiuliza nani alimuua chura,”.
Ilieleza wengi watajibu ni maji ya moto lakini ukweli ni kwamba ni kushindwa kwake kujua ni wakati gani aamue afanye lipi na kwamba alipaswa kuruka wakati ana nguvu za kutosha.
0 Comments:
Post a Comment