MSANII wa muziki nchini Nigeria, Davido amemdhamini mtoto wa miaka mitano, Ibeno kwa maisha yake yote baada ya kumsikia akiimba Wimbo wake mpya wa ‘IF’ na kumfungulia akaunti yenye thamani ya naila milioni 30.
Kwa mujibu wa ukurasa wa shamrock80 ambaye husimamia kazi za msanii hiyo, akiwa anapita gafla alisikia sauti ikiimba wimbo huo na ndipo alipokwenda kumuangalia alikuta ni mtoto wa miaka mitano anaimba.
Kutokana na hali hiyo aliwasiliana na Davido na kumueleza hali halisi ndipo walipoamua kutoa kiasi hicho cha fedha hasa baada ya kuangalia historia ya maisha ya mtoto huyo.
“Nilikutana na mama yake ambaye alidai ametelekezwa na mumewe na kumuachia watoto wawili huku Utibe akiwa mtoto wa pili. Lakini mama yake amepooza mguu na kwamba hufanya biashara ndogo ndogo ili kutafuta fedha za mahitaji ya nyumbani na kuwasomesha,”.
Hivyo kutokana na hali ambayo waliiona nyumbani kwa mtoto huo ndio maana wakaamua kumsaidia mtoto huyo ikiwemo kumpa kiasi hicho cha fedha na mambo mengine.
0 Comments:
Post a Comment