Friday, May 5, 2017

Kumbe Thandy nae anajali jamii yake?


MALKIA wa filamu nchini Afrika Kusini, Thandy Matlaila amepanga kufungua taasisi yake itakayokuwa ikitoa elimu kwa wasichana namna ya kuepukana na vishawishi ambavyo vitawaepusha na mimba za utotoni na magonjwa.
Thandy ambaye amekuwa akijipambanua kama mrembo wa uswazi aliyefanikiwa amesema taasisi hiyo itakuwa ikitoa elimu kwa muendelezo huku wakiwaambia madhara ya kutoka kimapenzi na wanaume wenye umri mkubwa.
“ Nimegundua kundi kubwa la wasichana hivi sasa limeingia kwenye mahusiano yasiyo rasmi wakiwa katika umri mdogo sana, kama sisi tumepewa uwezo wa kutoa elimu kwanini tusifanye hivyo? Umaskini hauwezi kumfanya mtu apoteze utu na thamani yake,” anasema Thandy.


0 Comments: