Friday, May 5, 2017

Hatimaye Kailyn amwanika Baba wa mwanae


MREMBO Kailyn Lowry ameweka mambo hadharani baada ya kumtaja Chris Lopez kuwa ndio Baba wa mtoto wake wa tatu aitwaye, Isaac Elliot.
Mrembo huyo ambaye alipata mtoto wa tatu mapema mwaka huu alificha juu ya nani ni Baba wa mtoto huyo huku akiishia kusema jina la Mwanaume huyo siyo muhimu sana kama mtoto jambo ambalo lilizua hisia tofauti kwa mashabiki wake.
“ Watu wengi mlitaka kujua juu ya Baba wa mtoto huyu ni wachache sana ambao walikuwa wakimfikiria mtoto. Ndio maana sikutaka kumueka hadharani, lakini sasa kwa wale mliokuwa na maswali juu yake nafikiri sasa mtakaa kimya,” anasema Kailyn.


0 Comments: