Saturday, April 29, 2017

Urembo wote ule kumbe mkubwa eeh!


UMRI unakwenda kumbe! Licha ya kuzidi kuonekana bado mrembo Veterani wa Nollywood, Stella Damascus amesherehekea miaka 39 tangu kuzaliwa huku akimshukuru mume wake, Daniel Ademinokan kwa kumuwezesha kufika hapa alipo.
Stella amesema miaka 39 aliyonayo imekuwa yenye baraka kwake licha ya kupitia changamoto nyingi kwenye kazi na maisha binafsi lakini anamshukuru Mungu ameweza kuwa imara na kufanya kazi kwa mafanikio makubwa.
“ Mume wangu, rafiki yangu na Bosi wangu kwenye filamu nakushukuru sana, sina maneno ya kusema navyojisikia lakini itoshe kusema kwamba wewe umekuwa sababu ya mimi kufanikiwa maisha mwangu, nawashukuru pia mashabiki na niwaahidi ubora mkubwa wa kazi,” alisema Stella.


0 Comments: