Saturday, April 29, 2017

Beverly eti nae anatoa ushauri

NI kama king’asti wa filamu Beverly Naya ameamua kuwa mama ushauri, hiyo ni baada ya kuamua kujirekodi akitoa elimu ya mahusiano na kutupia katika mitandao yake ya kijamii.
Ipo hivi, kupitia mtandao wa Snapchat, Beverly aliamua kufunguka na kutoa somo kwa wasichana wa kiafrika kuacha kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume bila kuwachunguza na kujua tabia zao kiundani.
Beverly alisema wanaume wamekuwa ni watu wanaojua kushawishi na kama msichana asipokuwa makini ni rahisi kunasa, “ Wasichana wenzangu wanaume wana njia nyingi za kutongoza mwanzoni atakuonesha mapenzi yote na wewe kujiona umepata, lakini unatakiwa kwenda mbali zaidi na kumchunguza, ukiona anafaa kuwa nae ukiona mzushi mtupie mbali,”


0 Comments: