Saturday, April 29, 2017

Rita kila siku anawaza mshiko aisee

KISURA Rita Dominic amezidi kupaa matawi ya juu baada ya kuachia jarida lake jipya ambalo litakua likihusisha maisha yake binafsi, uigizaji na urembo na kuwaomba mashabiki wake wamuunge mkono.
Rita amesema jarida hilo ni muendelezo wa mipango yake ya kuzidi kukuza jina lake katika tasnia ya filamu lakini pia kukuza thamani yake pamoja na kujiweka karibu na mashabiki wake ambao wamekuwa hawapati fursa ya kujua mambo mengi yanayomhusu.
“ Katika umri wangu huu wa miaka 41 natakiwa kuzidi kuwa mbunifu katika kufikiria biashara ambazo zitaniingizia kipato, sanaa ni kipaji change lakini inawezekana siku moja nikachoka na kushindwa kuigiza nahitaji kuwa na biashara za kumudu gharama za maisha,” anasema Rita.

0 Comments: