Wednesday, April 5, 2017

Staa wa filamu akiri kuona ukuu wa Mungu


TUMETOKA mbali aisee! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mrembo Angela Okorie kutupia mitandaoni picha zake za utotoni kipindi akiwa anaishi maisha magumu na kueleza jinsi gani Mungu alivyo mkubwa.

Angela ambaye ni mzaliwa wa Cotonou nchini Benin alianza maisha yake ya Sanaa mwaka 2009 ambapo hadio hivi sasa ameshiriki zaidi ya filamu 100 ambazo zimemfanya kuwa miongoni mwa waigizaji nyota nchini Nigeria.
“Hizi picha zimenikumbusha mbali na kunifanya nizidi kuona utukufu wa Mungu, nimetoka mbali kabla ya kuwa staa mkubwa wa filamu, mafanikio yangu yametokana na Baraka za Mungu na kamwe sitoacha kumshukuru,” anasema Angela.



0 Comments: