Wednesday, April 5, 2017

Mercy awaasa kuwa makini na mtandao wake

DIVA wa filamu za Nollywood, Mercy Johnson amesema kamwe hajawahi kumuachia mtu simu yake ili kupost vitu vinavyomhusu bali amekuwa akiandika mwenyewe na kwamba hata akaunti yake ya Facebook ni moja.

Kimwana huyo ametanabaisha hayo baada ya mashabiki wake kumtaka atolee ufafanuzi taarifa za kwamba ipo akaunti yeye jina lake ambayo inatumika kuwaomba mashabiki wake fedha jambo ambalo Mercy alilikanusha vikali.
“Nina simu moja tu ambayo naitumia peke yangu hakuna mtu ambaye nimewahi kumpa akaunti yangu anisaidie kuandika chochote, hivyo niwatake mashabiki wangu wasimsikilize mtu yeyote anaeomba fedha mtandaoni kwa kutumia jina langu,” anasema Mercy.



0 Comments: