Friday, April 28, 2017

Sir Elton augua ghafla alazwa Hospitali

MASHABIKI wa Gwiji la muziki Uingereza, Sir Elton John walikumbwa na simanzi na huzuni baada ya kuenea kwa taarifa ya kuugua ghafla kwa msanii huyo muda mchache kabla ya kufanya onesho lake mjini Las Vegas.
Veteran huyo alikuwa afanye shoo yake hiyo katika ukumbi wa Caesars Palace lakini ikashindikana baada ya kuugua huko kwa ghafla ambapo alilazwa Hospitalini kwa siku tatu kabla ya kuruhusiwa.
“ Nashukuru Mungu naendelea vizuri kwa sasa na niwatoe mashabiki wangu hofu hali imeimarika na imani yangu ni kwamba onesho letu lipo pale pale tutawatangazia tarehe,” anasema Sir Elton.


0 Comments: