Friday, April 28, 2017

Hii tabia haipendi kabisa Quick Rocka


RAPA na prodyuza, Quick Rocka ‘Switcher’ amedai kuna baadhi ya watu nchini wana tabia ya kumsubiri mtu akosee ili wamseme vibaya na sio kumshauri mapema ili asikosee.
Quick Rocka ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Down’, amewashauri wasanii wenzake kusikiliza kazi za zamani na siyo kusubiria ushauri.
“Watanzania wengi ni wakosoaji. Wasanii wengi wanaoharibu kazi huwa wanawaogopa wakosoaji na ndiyo maana utakuta wanaangaika kutengeneza muziki wa tofauti kumbe ndiyo wanaharibu.
“Mimi nawashauri tu kama watu wanataka muziki mzuri wasikilize nyimbo za zamani kisha wakitengeneze kazi zao yani hit song,” alisema Quick Rocka.


0 Comments: