Saturday, April 29, 2017

‘Acheni umbeya mtaniharibia kwa mpenzi wangu’

KAMA unafikiri kila Staa duniani anapenda skendo ili aendelee kuwa juu basi unajidanganya hivyo kwa, Amanda Manku, kimwana huyu ameamua kuwatolea povu wale wanaoneza ubuyu kuwa anatembea na Staa mwenzake, Kabelo Mahlasela.
Ripoti mbalimbali zinasanua ubuyu huo kuwa Amanda na Kabelo walionekana katika mikao ya kimahaba licha ya kuwa kwenye mahusiano na Staa wa Soka, Hendrick Ekstein.
“ Sijui hata hawa wanaoandika taarifa hizo wanazitoa wapi, sipendi kiki za kijinga ambazo zinaniharibia mahusiano yangu kwa Henfrick, ni jambo la kipuuzi kuandika kitu kisicho na ukweli, naombeni mniache jamani,” anasema Amanda.


0 Comments: