Friday, April 28, 2017

Ray atoa neno kuhusu Kanumba, Diamond

MUIGIZAJI Vincent ‘Ray’ Kigosi kutoka Bongo Movie amejikuta akikumbuka mambo ya kuumiza aliyokumbana nayo marehemu Steven Kanumba katika tasnia, na kueleza kwa sasa yanamnyemelea Diamond Platnumz.
Kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, Ray ameandika ujumbe mrefu  na kueleza hisia zake.
 “Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, mara anatumia nguvu za giza. Na kusema hata filamu zake hazikuwa nzuri lakini ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!.
“Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa sana na kuitwa bogus kwa madai hajui Kiingereza, Ni watanzania hawa hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. Lakini Leo wanamsifia hakuna kama Kanumba,” alianadika Ray na kuongeza.
“Diamond Platnumz nae baada ya kuona njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema ni Freemanson, wengine wanaonesha chuki ya wazi kwake. Wanasema hana muziki mzuri, mara ni kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema, hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa.
“Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! Hao ndio binadamu na tabia zao,” alisema Ray.
Aliongeza kuwa ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa uchawi wanageuza walichoamini.


0 Comments: