RAPA Nikki wa Pili amemtaja Msanii wa Rapa au Hip Hop ambaye anaimani ndio mwalimu wake wa muziki huo.
Katika mtando wake wa kijamii wa instagram, Nikki wa Pili alituma ujumbe uliombatana na picha ya Jay Z nakuandika “Mwalimu wangu bora wa somo la Rap”.
Ujumbe wa Nikki unakuja siku kadhaa mara baada ya Joh Makini kusema anajisikia faraja kwa mashabiki zake kumfananisha na Jay Z.
Joh Makini alisema ufananisho huo uko wazi kwa kuwa kiwango cha muziki wake ni mkubwa kiasi ambacho watu wanaomzunguka na wapenzi wa kazi zake hawaoni mtu mwingine wa kumfananishia naye isipokuwa msanii huyo kutoka ughaibuni.
“Jay Z ni ‘role model’ wangu, mimi naimba maisha ya sinoni daraja mbili na Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani, nafikiri nipo katika kiwango ambacho hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye,” alisema Joh Makini.
0 Comments:
Post a Comment