Saturday, April 29, 2017

Nnamdi na Jane mambo yamezidi kuiva

KISURA Jane Nnadozie amwaga mchele hadharani ili uliwe na kuku wengi, unaambiwa baada ya kudumu kwa muda mrefu kwenye uchumba yeye na mpenzi wake, Nnamdi Ezurike sasa wameamua kutangaza ndoa.
Wawili hao tayari wameweka wazi kuwa Ndoa yao itafanyika Mei, 6 Mwaka huu huku wakikataa kuweka hadharani sehemu sherehe hiyo itafanyika na mastaa wangapi wameshapewa kadi.
Jane ambaye ni mshindi wa Miss Asa Igbo mwaka 2014 amekuwa kwenye mahusiano na Nnamdi ambaye ni mfanyabiashara anaeishi Marekani.
“ Hatimaye tarehe zinazidi kukaribia, najua wapo waliotutakia mema katika mahusiano yetu na hatuna budi kutangaza kuwa tutafunga ndoa Mei 6, tunawapenda sana,” aliandika staa huyo wa filamu.


0 Comments: