RAPA kutoka Carlifonia, Marekani, Kendrick Lamar ni kama anazidi kuwafunga mkono wale wote waliokuwa wakimdiss kipindi anatoka baada ya kuweka rekodi ya mauzo ya albamu yake.
Albamu hiyo inayoitwa Damn imevunja rekodi ya mazuo iliyowekwa na Supastaa, Drake na albamu yake ya More Life iliyouza nakala 505, 000 kwa wiki ambapo hii ya Lamar imeuza nakala 603,000 kwa wiki na kukimbiza chati zote za muziki.
Staa huyo amekuwa na mafanikio tangu kutoka kwake ambapo Damn sasa inakua albamu yenye mauzo makubwa katika historia ya muziki ya Lamara ambapo albamu yake iliyopita ya Pimp a Butterfly iliuza nakala 324,000.
0 Comments:
Post a Comment