HII sasa sifa unaambiwa wakali wanaotamba na filamu ya The fate of the Fast 8, wanataka kuonesha umwamba wao kwa kuachia sehemu ya tisa ya filamu ili kukata kiu ya mashabiki wao ya kutaka kuona muendelezo wa muvi hizo.
Filamu hiyo ambayo imeweka rekodi ya mauzo kwa kuingiza kiasi cha Dola Milioni 523 ndani ya wiki moja imechezwa na wakali kama Dwayne Johnson ‘The Rocky’, Vin Diesel, Tyrese na wakali kama Ludacris ambao wamekuwepo katika filalmu za mwanzoni za Fast Furious sehemu ya kwanza hadi ya saba.
Sasa unajua sifa imekuja wapi? Unaambiwa baada ya kusikia tu kwamba wamevunja rekodi ya mauzo, mmoja wa wakali wa filamu hiyo Supastaa Tyrese akaamua kukinukisha kupitia Instagram yake baada ya kuweka kava la toleo jipya la filamu hiyo ambayo inatajwa kutoka 2019.
0 Comments:
Post a Comment