‘FIRST Lady’ wa lebo ya Wasafi, Zari the Boss amezidi kuwaonesha kina dada unaweza kuzaa na bado kuonekana mrembo baada ya kuachia picha zake akiwa katika muonekano mpya.
Inafahamika changamoto kubwa inayowakabili wanawake wengi pale wanapojifungua ni kulirudisha umbo lake, lakini kwa Zari imekuwa tofauti kwani licha ya kujifungua hivi karibuni ameweza kulirudisha umbo lake ndani ya kipindi kifupi.
Zari alijaribu kutoa somo kwa wanawake wengine kwa kuwaambia “ Unaweza kufanikiwa kurudisha umbo lako kama utazingatia nidhamu ya chakula na kufanya mazoezi, lakini unywaji wa maji mengi pia unahusika,”
0 Comments:
Post a Comment