Friday, February 24, 2017

Weeh! Kumbe Olomide yupo singo


Lagos, Nigeria
RAPA wa muziki nchini Nigeria, Olomide amesema kuwa bado hajawahi kuzama kwenye mahusiano ya mapenzi na mwanamke yoyote ingawa kwasasa ana mtoto mmoja wakiume.

Olomide ambaye ni mmoja wa nyota anayefanya vizuri nchini humo aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha Punch na alisisitiza kuwa yupo singo kwa miaka 17 sasa.

Alisema kuwa amekuwa akiogopa kuingia kwenye mahusiano kwakuwa anajua matatizo ya mapenzi na hivyo asingependa kuwa ni mmoja wa watu wanaojitumbukiza huko.

"Katika kazi yangu ya Sanaa naongopa sana kushuka na ninajua matatizo ya mapenzi hivyo nilichaguwa kuwa peke yangu hadi muda wangu utakapofika,"anasema.
Aidha anasema kitu pekee kitakachomrudisha kwenye mahusiano na wanawake ni ndoa.

0 Comments: